Na Saleh Ally
LUIS Suarez, leo hana ujanja na wala hawezi
kukwepa kwamba anatakiwa kufanya kazi ya ziada au kitu kitakachoushitua
ulimwengu kuonyesha sasa amerejea kwenye soka la ushindani.
Kifungo cha miezi minne kutokana na kumng’ata
beki wa Italia, Giorgio Chiellini kimepita. Pamoja na kuwaangalia nyota
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi watafanya nini leo kwenye mechi ya wapinzani
wakubwa, Real Madrid dhidi ya Barcelona ‘El Clasico’, bado Suarez atatupiwa
macho zaidi.
Wengi watamtupia macho Suarez ambaye atakuwa na
madeni kibao huenda kuliko Ronaldo na Messi au Gareth Bale na Neymar.
Suarez aliingia kwenye ‘pea’ ya tatu ya El
Clasico. Pea za klabu hizo mbili kongwe imejipanga hivi, ya kwanza ni Ronaldo
na Messi, inafuatia Neymar na Bale, halafu James Rodríguez na Suarez.
Pea ya tatu inakutana kwenye mechi hiyo yenye
rekodi zisizofutika na kila jambo linalofanyika kuanzia dakika ya kwanza hadi
ya mwisho linaingia kwenye rekodi.
Deni namba 1:
Barcelona ilikubali kumtwaa Suarez katika
kipindi cha matatizo, licha ya kuwa amefungiwa kwa kumng’ata Giorgio Chiellini
wa Italia, ikamsajili hivyohivyo kwa dau kubwa la pauni milioni 72 (Sh bilioni
187).
Deni namba 2
Barcelona walijiua Suarez amekosea, lakini
wakafumba macho na kuanza kumtetea kupita kiasi utafikiri alisingiziwa au
wakati Chiellini anang’atwa, Suarez hakuwepo!
Deni namba 3:
Ili acheze, lazima mchezaji mmoja akae benchi,
mfano Pedro Rodriguez. Kama akianzia benchi lazima mchezaji huyo acheze, hivyo
akiingia lazima aonyeshe kweli walikuwa sahihi kumuingiza.
Deni namba 4:
Mashabiki wa Barcelona nao ‘walijiwehusha’ kama
uongozi wao, wakamuunga mkono kupita kiasi, hivyo leo wataona faraja kubwa
akifunga bao ambalo litakuwa ni la kuwamaliza au kuchangia kuishinda Madrid
kwao Bernabeu.
Deni namba 5:
Barcelona imemchukua kwa kuwa msimu uliopita
ndiye alikuwa mfungaji bora England na Ulaya baada ya kufunga mabao 31.
Vipi atashindwa kufunga hata moja leo? Barcelona
inataka kuweka rekodi nzuri kwa kuwa tangu ianze kukutana na Madrid, Mei 3,
1902 imefunga mabao 364 wakati wenyeji wake hao wa leo wana mabao 384.
Anaweza kuwa na madeni lukuki katika siku yake
ya kwanza kuichezea Barcelona kwa kuwa ni kikosi kikubwa. Lakini ushindi dhidi
ya Madrid wakiwa nyumbani, ndiyo deni kuu ambalo mashabiki wa Barca wanataka
kuona likilipwa. Suarez ni mtukutu na ana uwezo mkubwa, bila ya kujali ataingia
au kuanza, bado ana nafasi ya kufanya vema.
TAKWIMU:
Real Madrid
Ushindi 91
Sare 48
Barcelona
Ushindi 88
Real Madrid - mabao 384
Barcelona - mabao 368
Jumla ya mechi 227
Takwimu za nyumbani:
Ushindi Sare Kupoteza
Madrid 65 25
25
Barcelona 63 23
26
SUAREZ, MZEE WA MAJANGA
Juni 2014 - Alimuuma Giorgio Chiellini
(akafungiwa miezi minne).
Aprili 2013 – Alimuuma Branislav Ivanovic
(Akafungiwa mechi 10).
Des. 2011 – Alitoa ishara mbaya kwa mashabiki
Fulham (akafungiwa mechi 1).
Des. 2011 – Alimbagua Patrice Evra (Akafungiwa
mechi 8).
Nov. 2010 – Alimuuma Otman Bakkal (Akafungiwa
mechi 7).
Julai 2010 –Alilambwa kadi nyekundu mechi dhidi
ya Ghana, kwa kushika makusudi katika Kombe la Dunia.
Nov. 2007 – Alizozana na wachezaji wenzake
(Ajax ikamsimamisha).
0 COMMENTS:
Post a Comment