Mwanasheria maarufu nchini, Dk Damas Ndumbaro
ameendelea kumuumbua Rais wa TFF, Jamal Malinzi baada ya kuonyesha asivyo
makini kwa mara nyingine.
Dk Ndumbaro ameonyesha uthibitisho wa kupokelewa
kwa rufaa yake ambayo siku moja tu Malinzi alisema Dk Ndumbaro hakuwa
amewasilisha rufaa yake ya kupinga kufundiwa miaka saba.
Katika ‘document’ hiyo inaonekana imesainiwa na
mmoja wa maofisa wa TFF na ilipokelewa tokea Oktoba 21.
“Sasa unaona kama Malinzi hajui hii document
imepokelewa ofisini kwake.
“Tena kabla ya kuuliza anakwenda kutoa taarifa
kwenye vyombo vya habari. Hii ni sehemu ya kuonyesha si makini.
“Kesi yangu ilisikilizwa ndani ya siku nne,
lakini leo ni zaidi ya wiki, rufaa yangu haijasikilizwa na nimeishalipa TFF
shilingi milioni moja ya rufaa.
“Haya yote yamefanyika ofisini kwa Malinzi lakini
yeye halijui hilo,” alisema Dk Ndumbaro akionyesha kujiamini.







Tatizo lako saleh ni elimu duni na ufahamu wa sheria uliokuwa nao.
ReplyDeleteHapo hakuna rufaa iliyokatwa kisheria hiyo document inaonyesha kusudio la rufaa na vipengele vya hiyo rufaa na si rufaa kisheria.Poor you!
Kweli nimegundua watanzania wengi hasa hawa wakamata kalamu ni mambumbumbu wa sheria na hata kimalkia kimewapita njiani!
ReplyDeleteYaani Memorandum of Appeal mtu anaandika na kukomalia eti Ngumbaro kakata rufaa,aibu iliyoje?!
Saleh Ally unatuaibisha ndugu zako!