Wakati Kocha Msaidizi, Leonardo Leiva alilambwa kadi
nyekundu katika mechi ya Yanga dhidi ya Kagera, bosi wake amesema wachezaji wa
timu hiyo ya Bukoba waliharibu mchezo kwa kupoteza muda.
Marcio Maximo amesema Kagera walipoteza muda makusudi
katika mechi yao ya Ligii Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba, jana.
“Walipoteza sana muda, mwamuzi ameona hiyo hali lakini
ajabu kaongeza dakika tatu tu.
“Haikuwa sahihi na hii si haki hata kidogo. Imenishangaza
sana, nafikiri mnafurahia kuona Yanga inapoteza,” alisema Maximo.
Yanga ililala kwa bao 1-0 katika mechi hiyo dhidi ya
Kagera ikiwa nyumbani.







0 COMMENTS:
Post a Comment