Mechi inakaribia kuanza, tayari wachezaji wa Liverpool na Chelsea wameanza kupasha misuli kwenye uwanja wa Anfield.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu England inatarajia kuwa na mvutano mkubwa licha ya Liverpool kuonekana hawako imara sana.
Kawaida mechi kubwa huwa zinabadilika ingawa takwimu zinaonyesha kiungo cha Chelsea kinachoongozwa na Nemanja Matic na Cesc Fabregas ni imara zaidi katika ukabaji na ushambulizi.
Pia safu yao ya ushambuliaji ni kiwembe na hasa washambuliaji wanne, Diego Costa, Didier Drogba, Oscar na Eden Hazard.
Lakini vipi utawadharau Liverpool wenye watu kama Mario Balotelli, Rahim Sterling, Emre Can, Steven Gerrard, Adam Lallana na wengine.
Inawezekana wakazidiwa kimfumo lakini bado uwezo wa mchezaji mmoja mmoja unaweza kuwa tatizo kwa Chelsea.
Kawaida Chelsea inataka kutangulia na takwimu inaonyesha ndiyo timu ngumu zaidi kuifunga bao la kusawazisha, lakini katika soka kila dakika 90 ina mambo yake.
Hivyo ni mechi bora ya kutazama na ikiwezekana tulia na itazame kwa jicho la pili, si lile la kishabiki.
Mechi njema mdau.
0 COMMENTS:
Post a Comment