Uongozi
wa Mbeya City umesema kupoteza mechi tatu mfululizo haliwezi kuwa jambo
litakalowavuruga.
Badala
yake, Mbeya City wamesisitiza watakuwa wakifanya mambo yao kutatua matatizo.
Msemaji
wa Mbeya City, Dismas Ten amesema tayari Kocha Juma Mwambusi amekuwa akifanya
marekebisho kabla ya mechi dhidi ya Stand United mjini Shinyanga.
“Tayari
tuko Shinyanga, jana tulicheza mechi ya kirafiki na leo kocha amekuwa
akimalizia maandalizi.
“Kupoteza
hakuwezi kutufanya tuanze kulumbana na kulaumiana. Tumemuachia kocha afanye
anachoona ni sahihi.
“Bado
tunaamini tutarudi katika njia sahihi na kuendelea kupambana,” alisema Dismas
Ten.
0 COMMENTS:
Post a Comment