Msemaji
wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru haishi maneno lukuki, safari ameibuka na jipya.
Amesema
kuwa kikosi cha Mtibwa Sugar hakitapoteza mechi yoyote.
“Mechi
yetu inayofuata ni dhidi ya Kagera Sugar ndugu yangu. Itakuwa ngumu kwa kuwa
hawa ndugu zetu kutoka Akagera ni wagumu na wana uwezo mzuri.
“Lakini
ninachokuambia Mtibwa Sugar haitapoteza mchezo msimu huu. Kazi yetu ni kutoa
vipigo hadi mwisho,” alisema.
“Lengo
ni kuwa mabingwa na tutakuwa mabingwa, tulia uone.”
Hadi
sasa katika mechi sita, Mtibwa Sugar haijapoteza hata moja baada ya kushinda
nne na kutoka sare mbili.
0 COMMENTS:
Post a Comment