Mshambuliaji Lionel Messi
amefanikiwa kuifikia rekodi ya nyota wa zamani wa Real Madrid katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Raul alikuwa akishikilia
rekodi ya kufunga mabao 71 na kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi kwenye
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Licha ya kwanza Cristiano
Ronaldo alionekana ndiye atakuwa wa kwanza kumfikia Raul, lakini mabao mawili
aliyofunga Messi wakati Barcelona ikiitwanga Ajax kwa mabao 2-0 kwenye mechi ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya, yamesitisha ndoto za Ronaldo.
Messi amefikisha mabao 71
huku Ronaldo akibaki na mabao 70 na anachotakiwa sasa ni kufunga zaidi ili
kumfikia Messi na Raul na ikiwezekana kuwapita.
NAMBA MOJA:
Lionel Messi (Barcelona) - mabao 71;
Raul (Real Madrid, Schalke) - 71
NAMBA MBILI:
Cristiano Ronaldo
(Manchester United, Real Madrid) - 70
NAMBA TATU:
Ruud van Nistelrooy (PSV
Eindhoven, Manchester United, Real Madrid) - 56
NAMBA NNE:
Thierry Henry (Monaco,
Arsenal, Barcelona) - 50
0 COMMENTS:
Post a Comment