NUNEZ |
Rais wa zamani wa Barcelona, Josep Lluis Núñez amehukumiwa
jela miaka miwili na miezi miwili.
Nunez ,83, anaingia jela akiongozana na mwanaye Josep
Lluis Núñez i Navarro ambaye atatumikia kifungo kama hicho, wote wawili wakiwa
wamepatikana na hatia ya kukwepa kodi.
NUNEZ (KUSHOTO), KULIA NI MWANAYE JOSEP, WOTE WAWILI WAMEHUKUMIWA MIAKA MIWILI NA MIEZI MIWILI. |
Nunez na mwanaye walikata rufaa, lakini baadaye
ikatupiliwa mbali.
Hivyo wawili hao wameanza kutumikia kifungo katika jela
ya Quatre Caminos katika jimbo la La Roca del Vallès katika Manispaaa ya jiji
la Barcelona.
Hata hivyo imeelezwa bado wana mpango wa kukata tena
rufaa kuhusiana na huku hiyo.
Nunez alikuwa Rais wa Barcelona katika vipindi tofauti
kuanzia mwaka 1978 hadi 2000.
Wakati akiwa kiongozi kwa nyakati hizo tofauti,
aliiwezesha Barcelona kupata mafanikio makubwa.
Nunez aliiwezesha Barcelona kubeba makombe yafuatayo:
7-La Liga
6-Copa del Rey
5-Spanish Super Cup
1-Ligi ya Mabingwa Ulaya
4-Kombe la Washindi Ulaya
2-Uefa Super Cup
0 COMMENTS:
Post a Comment