Washambuliaji
wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, tayari wameungana na kikosi
cha Taifa Stars.
Stars imeweka
kambi jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini kujiandaa na mechi ya kirafiki
dhidi ya Swaziland, wikindi hii.
Wachezaji hao
pekee ndiyo waliobaki kuungana na wenzao na walipanda ndege moja kwa moja
kutoka Lubumbashi, DR Congo.
Stars
itacheza mechi hiyo iliyo katika kalenda ya Fifa ambayo faida yake ni kupanda
kwenye viwango vya shirikisho kama itashinda.
Mechi ya mwisho
ya kirafiki jijini Dar es Salaam, Simba iliitungua Benin kwa mabao 4-0.
Tanzania na Benin ni 4-1 sio 4-0
ReplyDelete