August 4, 2018


Kocha pekee mwenye uraia wa Ufaransa na DR Congo kwenye Ligi Kuu Bara, Mwinyi Zahera anayeinoa Yanga amesema anaona wazi kwamba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linataka kuibeba Simba msimu ujao wa ligi kuu kutokana na ratiba kuwa rafiki kwao.

Ratiba ya ligi kuu ambayo imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22, inaonyesha Yanga itaanzia ugenini katika michezo yake mitatu ya ugenini ambapo ni dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro itakayopigwa Agosti 23, kisha watakwenda Bukoba kuvaana na Kagera Sugar Agosti 25 halafu Septemba 2, watakwenda Shinyanga kucheza na Mwadui FC.

Lakini hata hivyo Yanga baada ya kucheza mechi na Kagera Agosti 23, watalazimika kuanza kujiandaa na safari ya kwenda Rwanda ambapo watakuwa na mechi ya hatua ya makundi ya Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports.

Simba yenyewe itacheza mechi tatu nyumbani ambazo ni dhidi ya Prisons itakayopigwa Agosti 22, kisha Agosti 25 watacheza na Mbeya City halafu Septemba Mosi watakipiga na Lipuli.

Hivi karibuni TFF ilitangaza kuwa timu mwenyeji ndiyo itakayokuwa inachukua mapato yote hali ambayo Yanga wanaona kama wanaonewa kwani hawatopata chochote kwenye mechi hizo.

Kutokana na ratiba hiyo, Zahera amesema anaona wazi kuwa TFF inataka kuibeba Simba kwani haiwezekani wao wakapangwa kucheza mechi tatu mfululizo ugenini tofauti na ilivyo kwa Simba na Azam ambao ni wapinzani wao wa karibu ambao wao watacheza mechi tatu nyumbani.

“Ni mara ya kwanza kuona kitu hiki kinatokea dunia nzima, huwezi kuanza kucheza mechi tatu ugenini huku wenzako ambao mnapigania kuwania kombe wanaanzia nyumbani.

“Hii inaonyesha wazi kuwa TFF inaisaidia timu ya Simba, sijui kwa nini wamefanya hivi inaumiza kwa nini Azam na Simba waanzie nyumbani mechi tatu na sisi ugenini tu, kuna sababu gani,” aliwaka Zahera.

CHANZO: CHAMPIONI

24 COMMENTS:

  1. Basi Tff kama wataweza wawafanyie Yanga wacheze mechi zao zote nyumbani..maana sasa kila kitu wanaolala kuonewa..mbona Mbeya city na prison hawalalamiki au wao hawagombanii kombe..

    ReplyDelete
  2. huyo kocha hata bado hajakutana na Simba tayari ameanza visingizio

    ReplyDelete
  3. ila hili la timu mwenyeji kuchukua mapato wamejitakia wenyewe wote tunajua Simba na Yanga mechi zao za mkoani ndio zinajaza watu zaidi ilikuwaje wakapitisha kanuni hii

    ReplyDelete
  4. Huyu kocha nampa pole sana hajakumbana na kipigo cha simba anaanza kupiga kelele we subiri time....

    ReplyDelete
  5. Kocha huyu atapata taaaabu saaana. TFF hebu rekebisheni ratiba Yanga icheze mechi 5 za mwanzo nyumbani uwanja wa taifa.

    ReplyDelete
  6. Naona comment zote zimejaa ushabiki hii sio Fair play katika mpira ligi gani duniani inayopanga ratibu ya hovyo kama hiyo kwa vile upende mnaoushabikia unanufaika mnaona sawa

    ReplyDelete
    Replies
    1. nadhani walipaswa kuomba ratiba iwe rafiki kwao kwa mihuano ya Kombe la shirikisho lakini kitendo cha kuanza kulalalika kuwa kuna upendeleo mi naona hawako sawa, they need to focus on theirs and not otherwise.

      Delete
    2. Mkuu watanzania hatuna muda wa kufikiri maendeleo ama kujibu hoja zaidi ya ushabiki

      Delete
    3. siku zote wabongo hawajwahi kuwaza positive ni ushabiki ushabiki tuuu, fuatilia ligi zote hakuna mtu anapewa mechi tatu zote ugenini lazima huwa kunakuwa na mabadiliko , home and away ...hii inatokea Tanzania kwa viongozi wasio na akili kama wa TFF

      Delete
    4. Sio kweli kuwa ni pekee duniani. Angalia epl kuna timu ambazo zinacheza away mara mbili mpaka tatu wakati mwingine. Hoja hapa ni kuongelea timu yao sio Simba. Ligi yetu haina pesa ndo mana timu ikitoka inapewa unafuu wa kucheza mara kadhaa ili kupunguza gharama za kwenda na kurudi. Hata hao simba na azam wataenda ugenini mara tatu. Njaa ndo inasumbua tu hapo, wangekuwa na pesa wangeanza kushangilia kuwa wanaanza ugenini hivyo watamalizia nyumbani. Msijitekenye halafu mnacheka wenyewe.

      Delete
  7. mbona azam hawaongelei huo ni uwoga wa kuiogopa simba

    ReplyDelete
  8. Kocha huyo anajieekea kinga ili atapoanza kupata vipigo hiyo ndio sababu zake. Idadi ya mechi yanga itayozicheza ugenini ni sawa na timu zote. Ikiwa yeye anaogopa kuchapwa ugenini basi na Simba pia itachapwa ugenini. Huyu kocha anaonesha moga sana hadi anakiogopa kivuli chake mwenyewe. Maneno yake yatawayisha wachezaji wake na kuwavunja moyo na kupoteza muelekeo.

    ReplyDelete
  9. Wako wanaojidhani wako salama na ratiba inayolalamikiwa na mtaalamu iko siku tutawasikia wakilialia na kusahau waliyoyaandika wakati huu

    ReplyDelete
  10. Yanga acheni kulia kia buana..kila kitu mnafanyiwa nyie..mchezaji hamjamsajili mnalia mmenyang'anywa..mliona wapi duniani mchezaji anawania na timu moja.. kwa woga huo..na simba hii jiandaeni kisaikolojia..

    ReplyDelete
  11. Kiasi fulani timu inapoanza ugenini ni faida kubwa nashsngaa kocha huyo analalamika hovyo bila ya point. Anachotakiwa kufahamu Simba ya sasa ni mpinzani wa yanga kwa maneno tu lakini kiukweli Simba imeshasogea na ipo level nyengine. Isitoshe Simba ndie bingwa wa ligi lazima apewe heshima yake. Yanga mshindi wa nne sijui wa tano wanataka kuwa na heshima sawa na bingwa? Yanaga wamezoea kubebwa na huyu kocha anatafuta ubaya na TTF. Kuna uwezekano huyu kocha akakimbia kabla ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuisha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. THINK POSITIVEm speculate before you alter

      Delete
  12. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
    Replies
    1. This comment has been removed by the author.

      Delete
  13. siku zote wabongo hawajwahi kuwaza positive ni ushabiki ushabiki tuuu, fuatilia ligi zote hakuna mtu anapewa mechi tatu zote ugenini lazima huwa kunakuwa na mabadiliko , home and away ...hii inatokea Tanzania kwa viongozi wasio na akili kama wa TFF

    ReplyDelete
  14. Ijadiliwe hoja, wahenga wapumzike kwa Amani.
    Zamani mechi moja Dar, kigogo mwingine mikoani kigogo kikirudi kingine kinaondoka.

    Hadi Raha Leo timu inaweka kambi Dar/mkoani

    Si upendeleo ni uvivu, na kutojua wananchi shughuli na nacho.

    ReplyDelete
  15. Ijadiliwe hoja, wahenga wapumzike kwa Amani.
    Zamani mechi moja Dar, kigogo mwingine mikoani kigogo kikirudi kingine kinaondoka.

    Hadi Raha Leo timu inaweka kambi Dar/mkoani

    Si upendeleo ni uvivu, na kutojua wananchi shughuli na nacho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic