Beki
wa kati wa Azam FC, Aggrey Morris, amemvulia kofia kiungo mshambuliaji wa
Yanga, Simon Msuva na kusema kuwa hakabiki kirahisi ni bora atimkie Ulaya kwani
uwezo wa kucheza anao.
Beki
huyo alimwaga sifa hizo baada ya kumalizika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya
timu yake na Yanga ulioisha kwa sare ya mabao 2-2 ambapo Msuva alionekana mwiba
kutokana na kusumbua ukuta wa Azam uliokuwa chini ya Serge Wawa na Morris.
Mchezo
huo ulipomalizika mashabiki wa Yanga walionekana kuikubali timu yao licha ya
matokeo hayo kutokana na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na timu hiyo
inayonolewa na Kocha, Mdachi, Hans van Der Pluijm.
Beki huyo anayecheza ‘kazikazi’ alisema mchezaji
aliyempa wakati mgumu katika mchezo huo ni Msuva licha ya uwepo wa mastraika wa
kigeni Mliberia, Kpah Sean Sherman pamoja na Mrundi, Amissi Tambwe.
“Mchezaji
mzuri ni yule anayejua kukaa katika ‘position’ mzuri, mastraika wa Yanga
wamecheza vizuri, hasa yule Mliberia na Tambwe ingawa hawakunipa shida sana.
“Kwangu
aliyenisumbua ni Msuva, jamaa anajua sana, yani akikupita tu basi,
kinachotakiwa ni kumalizana naye haraka anapokuwa na mpira. Ninafikiri ana
uwezo mkubwa anaweza kucheza soka hata Ulaya akipata nafasi,” alisema Aggrey.
0 COMMENTS:
Post a Comment