NYOSSO WAKATI AKIWA COASTAL, AKIPAMBANA NA KAVUMBAGU ALIYEKUWA YANGA. |
Beki wa kati wa Mbeya City,
Juma Said Nyosso ‘Baba Saidi’ amefunguka kuwa hawahofii washambuliaji wa Yanga,
Amisi Tambwe, Kpah Sherman na Danny Mrwanda katika mchezo watakaokutana baada
ya Yanga kutoka kwenye Kombe la Mapinduzi.
Nyosso aliiongoza Mbeya
City kuibuika na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara, katika mchezo
uliochezwa wikiendi iliyopita ikiwa ni ushindi wa pili tangu ligi ianze.
Yanga na Mbeya City
zitakutana katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, katika mchezo wa raundi ya tisa wa
Ligi Kuu Bara.
Nyosso alifunguka kuwa hawahofii washambuliaji wa Yanga akiwemo Tambwe,
kwa kuwa kazi yake ni kuhakikisha timu yake hiyo inashinda michezo yote iliyopo
mbele yao.
“Nashukuru Mungu kuona
tumeanza vizuri, kwenye ligi kwa kushinda bao moja dhidi ya Ndanda na tayari
nimeshaelewana na mabeki niliowakuta kwani lengo letu ni kuhakikisha tunapata
ushindi katika kila mechi.
“Tumejiandaa kwa ajili ya
mechi zote za ligi na si Yanga pekee kwa kuwa lengo letu ni kuona timu inakuwa
kileleni.
“Kwa muda mfupi niliokaa na
wachezaji wezangu tayari tumeshaelewana na nipo vizuri hata mechi dhidi ya
Yanga hakika simhofii Tambwe wala mchezaji yeyote wenyewe waje tu wataona kazi,”
alisema Nyosso.
0 COMMENTS:
Post a Comment