Baada ya kucheza mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara chini ya Kocha, Mholanzi, Hans van Der
Pluijm, kiungo mchezeshaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, ameibuka na kusema
anaufurahia mfumo wa kocha huyo kwa kuwa unaifanya timu kucheza kwa kushambulia
zaidi.
Kiungo
huyo raia wa Rwanda alisema kuwa kocha aliyepita Mbrazil, Marcio Maximo alikuwa
anataka zaidi soka la kushambulia kwa kushtukiza, lakini Pluijm anasistiza soka
la pasi fupi, kasi na kushambulia muda wote, kitu ambacho ni kizuri kwani
kinawapa presha wapinzani.
Niyonzima
aliongeza kuwa yeye ‘ameupata’ haraka mfumo wa kocha huyo kwa sababu si mgeni
katika kikosi cha Yanga, pia ndiyo aina ya mfumo unaomfanya acheze ‘atakate’
kwa sababu anapenda soka la kushambulia zaidi.
“Kukopi
mfumo kwa haraka ni ngumu, lakini mwalimu huyu (Pluijm) si mgeni sana kwetu,
labda baadhi ya wachezaji wachache ambao hawakuwepo awali akifundisha Yanga.
“Mfumo
wake ni mzuri unatufanya tucheze pasi na kushambulia kwa haraka tofauti na
Maximo ambapo tulikuwa tukitumia zaidi ‘kaunta ataki’ na kukaba sana ili
wapinzani wasipate nafasi.
“Mfumo
wa kushambulia ni mzuri zaidi kwa sababu lengo la timu ni kuchukua pointi tatu,
sasa unaposhambulia muda mwingi unawapa presha wapinzani na kufanikiwa kupata
unachokitaka,” alisema Niyonzima ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment