Wakati
raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inakamilika leo (Desemba 29 mwaka
huu) kwa mechi tatu, ligi hiyo itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa
mechi tano.
Coastal
Union itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting
itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Azam itakuwa mwenyeji wa
Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex, Stand United itakuwa mgeni wa
Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City na Yanga
zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.
Ligi
hiyo ambayo itachezwa mfululizo (non-stop) hadi itakapomalizika Mei 9 mwakani,
itakamilisha raundi ya tisa Januari 4 mwakani kwa mechi kati ya Mgambo Shooting
na Simba kwenye Uwanja wa Mkwakwani, na Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji
wa Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine.
Nayo
mechi kati ya Mtibwa Sugar na Stand United ambayo jana ilivunjwa na mvua dakika
ya 6 imemaliziwa leo ambapo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Wakati
huo huo, mechi ya ligi iliyochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex
imemalizika kwa wageni Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT
Ruvu. Bao hilo lilifungwa kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na
Hamisi Kasanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment