Timu
ya Mbao FC ya Mwanza imekamata uongozi wa Kundi B la michuano ya Ligi Daraja la
Pili (SDL) baada ya jana (Desemba 27 mwaka huu) kuizamisha JKT Rwamkoma ya Mara
mabao 2-1.
Kwa
matokeo hayo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mbao FC
imeitoa kileleni JKT Rwamkoma baada ya kufikisha pointi tisa kwa kushinda mechi
zote tatu dhidi ya Arusha FC, Pamba na JKT Rwamkoma.
Mbao
FC inafuatiwa na JKT Rwamkoma yenye pointi sita, Arusha FC pointi sita wakati
Bulyanhulu na Pamba zikiwa za mwisho kwa pointi moja kila moja. Kundi hilo
litakamilisha mzunguko wa kwanza Januari 3 mwakani kwa mechi kati ya JKT
Rwamkoma na Arusha FC, na Bulyanhulu na Mbao FC.
Katika
kundi A, Mji Mkuu (CDA) na Singida United ndizo zinazochuana kileleni kwa
kufikisha pointi saba kila moja. Timu hizo zinafuatiwa na Milambo yenye pointi
nne, Mvuvumwa FC yenye pointi moja wakati Ujenzi Rukwa ni ya mwisho ikiwa haina
pointi.
Hata
hivyo, Mvuvumwa FC na Milambo ziko nyuma kwa mechi moja. Mechi hiyo ya
kukamilisha raundi ya tatu kati ya timu hizo itachezwa kesho (Desemba 29 mwaka
huu) kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Kiluvya
United imeendelea kuchachafya kundi C baada ya kushinda mechi zote ne
ilizocheza, hivyo kufikisha pointi 12. Inafuatiwa na Mshikamano yenye pointi
saba huku Abajalo ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 6.
Nafasi
ya nne inashikwa na Transit Camp yenye pointi nne, Cosmopolitan yenye pointi
mbili ni ya tano wakati Kariakoo ambayo haina pointi ni ya mwisho. Hata hivyo,
Cosmopolitan na Kariakoo zina mchezo mmoja mkononi.
Mechi
zinazofuata za kundi hilo ni Januari 3 mwakani kati ya Kariakoo na Mshikamano
na Mshikamano (Ilulu), Transit Camp na Abajalo (Mabatini), na Cosmopolitan na
Kiluvya (Karume).
Kundi
D, vinara bado ni Njombe Mji yenye pointi 12 ikifuatiwa na Wenda yenye pointi
sita wakati Volcano FC iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano. Mkamba Rangers
ina pointi nne, Town Small Boys ina pointi moja wakati Magereza FC haina
pointi.
Katika
kundi hilo leo (Desemba 28 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Town Small Boys
na Magereza itakayochezwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Januari 3 mwakani kutakuwa
na mechi kati ya Town Small Boys na Njombe Mji, Volcano FC na Magereza, na
Wenda na Mkamba Rangers.
0 COMMENTS:
Post a Comment