Klabu ya Polisi Moro imeingia mkataba wa mwaka
mmoja na aliyekuwa kiungo wa Simba, Zahoro Pazi.
Kiungo huyo aliwahi kukipiga katika klabu
za Mtibwa Sugar na Simba sasa ataanza kuonekana na kikosi cha Polisi.
Msemaji wa Polisi
Moro, Clement Bazo, alisema kuwa wameamua kumsajili kiungo huyo kutokana na
uwezo wake na wanaamini kuwa atawasaidia kwa kiasi kikubwa.
Bazo alisema kuwa kwa sasa kikosi chao kinaendelea na mazoezi
na wachezaji wanaoachwa katika kikosi hicho watatangazwa hivi karibuni.
“Tumemsajili Kiungo Zahoro Pazi ambaye aliwahi kuitumikia Simba msimu
uliopita, tunaamini uwezo wake na
umahiri alionao utaweza kuisaidia timu yetu kwa kiasi kikubwa msimu huu
kwa sababu lengo ni kufanya vizuri.
“Na kama inavyofahamika ushindani umekuwa
mkubwa sana, kila timu inajitahidi kuonyesha na kuhakikisha inafanya vyema na
ili kuwa na kikosi bora kuna wachezaji takribani watano lazima watapigwa panga
ili kuboresha kikosi,” alisema Bazo.







0 COMMENTS:
Post a Comment