![]() |
| SEHEMU YA ENEO LA HOTELI WATAKAPOWEKA KAMBI YANGA. |
Bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Marcio Maximo, amesema ana uhakika wiki moja itamtosha
kabisa kufanya kweli dhidi ya watani wao, Simba ambapo timu hizo zitakutana
Jumamosi wiki hii kwenye mchezo wa Bonanza la Nani Mtani Jembe.
Yanga wanatarajia kuingia kambini leo Land
Mark Bahari Beach kujiwinda na mchezo huo ambao watakuwa wakihitaji kulipa
kisasi kufuatia mwaka jana kukubali kichapo cha mabao 3-1.
Maximo
alisema kuwa kikosi chake kimejipanga vema ambapo anaamini kambi ya wiki moja
inawatosha kabisa kujiweka fiti zaidi dhidi ya Simba.
“Tuna muda mfupi kabla ya mchezo ambao naweza
kusema ni mgumu lakini naamini wiki moja inatosha kabisa kujiweka sawa zaidi
kwa ajili ya mchezo huo,” alisema Mbrazili huyo.
Kichapo cha Yanga mwaka jana kilisababisha kuvunjwa
kwa benchi zima la ufundi lililokuwa likiongozwa na Mholanzi, Ernie Brandts na
Fred Felix Minziro.








0 COMMENTS:
Post a Comment