Mabingwa wa Ligi Kuu Bara mwaka 1988,
Coastal Union, wameamua kupata mechi moja ya kirafiki ya kimataifa, ambapo jana
walitarajia kumenyana na Mombasa Kombaini mjini Mombasa, Kenya kabla ya kurejea
tayari kuwavaa Wajelajela wa Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu
Bara utakaopigwa Desemba 27.
Kikosi hicho kinachonolewa na kocha
mpya, Mkenya, James Nangwa pamoja na kocha wa zamani wa Yanga, Mfaume Athuman,
kilipaa jana kwa ajili ya mechi hiyo ili kupima uwezo wao kabla ya kukwaana na
kisiki Prisons ambayo huaminika kuwa imara inapocheza kwenye Uwanja wa Sokoine,
Mbeya.
Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga, alisema ziara yao ilitokana na
matakwa ya benchi la ufundi.
“Mbali na hilo pia tunataka kuwajaribu
wachezaji wetu kama akina (Abdulhalim) Humud ambao walisajiliwa katika dirisha
dogo msimu huu, pia benchi la ufundi linataka kuutumia mchezo huo kubaini
kasoro zilizopo baada ya kukaa kambini muda mrefu,” alisema Assenga.
Coastal na Prisons zina
kumbukumbu ya kutoka suluhu katika
mechi zote mbili msimu uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment