December 5, 2014

KIFARU (KUSHOTO) AKIMSISITIZIA SALEH ALLY KWAMBA MTIBWA SUGAR, ITABEBA UBINGWA.
Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amemuambia mwandishi mkongwe wa michezo nchini, Saleh Ally maarufu kama Jembe atulie na kuona Mtibwa Sugar inavyokuwa bingwa.


Saleh alimuuliza Kifaru kuhusiana na suala kama kweli wanaweza kuendelea na kasi yao baada ya ligi kusimama, itakapoanza, wataweza kuendeleza libeneke.

Naye akamjibu:
"Tulia Saleh, Mtibwa Sugar ndiyo mabingwa wapya wa Tanzania Bara. Hii haitakuwa mara ya kwanza, lakini ujue pamoja na kwamba tumefanya vizuri kwenye mechi saba.

"Bado vijana wanajituma hakuna aliyebweteka kwa kuwa tunajua ushindani ni mkali sana."

Mibwa Sugar ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara na hadi sasa hawajapoteza hata mchezo mmoja.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic