Kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
amewavaa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kitendo cha
kubadilisha waamuzi bila ya sababu za msingi.
Hayo
yamekuja baada ya mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya Mwadui FC na Toto
Africans uliopigwa juzi kubadilishwa waamuzi siku moja kabla ya mchezo huo,
hivyo Julio kulichukulia hilo kama hujuma dhidi ya timu yake ingawa
walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Julio amesema kuwa kitendo
cha kubadilishwa waamuzi kimyakimya hakileti picha nzuri, hivyo wahusika
wanatakiwa kulitazama hilo kwa jicho la tatu, alisisitiza kuwa TFF wasiwe na
timu wanayotaka ipande badala yake waache kila timu ipande kwa uwezo wake.
“TFF
ndiyo baba wa soka, kwa hiyo wahakikishe wanafuata kanuni na utaratibu wa
kuongoza soka. Inakuwaje waamuzi wanabadilishwa siku moja kabla ya mchezo, tena
usiku? Huoni hapa kama kuna ujanja-ujanja unajaribu kutengenezwa?
“TFF
waliangalie sana hili, linaharibu mpira wetu. Waamuzi wale walibadilishwa kwa
lengo lipi? Sisi hatujui. Wasitake kulazimisha timu fulani ipande, waache timu
ipande kwa uwezo wake na si kubebwa-bebwa,” alifoka Julio.
Alipotafutwa
Ofisa wa Ligi, Joel Balisidya, kwa njia ya simu kulizungumzia suala hilo jana
Jumapili hakupatikana huku ofisi za bodi hiyo zikiwa zimepigwa kufuli.
0 COMMENTS:
Post a Comment