December 6, 2014




Klabu ya Mtibwa Sugar inatarajiwa kuondoka siku ya Jumanne kuelekea jijini Mbeya wilayani Kyela ambapo huko watacheza michezo ya kirafiki na timu za Super Ligi za nchini Malawi ambapo TFF imetoa baraka katika hilo baada ya kupata mwaliko kutoka Chama cha Soka Wilaya ya Kyela.


Mtibwa mpaka sasa inashikilia nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 15 na kwa sasa timu zipo katika maandalizi kuelekea ligi kuu.

Ofisa habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru alisema kuwa wakiwa huko wataendelea na mazoezi na kucheza michezo ya kirafiki na timu tofauti za Ligi Kuu ya Malawi kisha watakwenda Songea mkoani Ruvuma.


“Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa tunajenga na kuimarisha kikosi chetu kuwa na ushindani zaidi pindi ligi itakapoendelea ili kuweza kuwa katika nafasi nzuri ligi inapokuwa inamalizika,” alisema Kifaru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic