Mshambuliaji mpya wa Simba, Mganda Dan Sserunkuma, anatarajiwa kutua nchini kesho Jumapili
na kujumuika na wenzake Jumatatu ijayo kwa ajili ya kuendelea na programu za
mazoezi ya timu hiyo.
Sserunkuma
aliyesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia
inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, aliondoka nchini hivi karibuni na kurejea
nyumbani kwao mara tu baada ya kumalizana na klabu yake mpya ambapo alienda
kuchukua vifaa vyake.
Katibu wa Simba, Stephene Ally, alisema mchezaji huyo
anatarajia kutua nchini kesho kabla ya kuungana na wenzake mazoezini siku ya
Jumatatu (keshokutwa).
“Sserunkuma
alienda kwao Uganda na tunatarajia atatua nchini Jumapili (kesho) hii tayari
kwa kuanza kazi na klabu yake mpya ambapo atakuwa mazoezini siku inayofuata
lakini bado hatujafahamu atakuja na ndege gani,” alisema Ally.
Simba
kwa sasa inajiandaa na mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Yanga itakayopigwa
Jumamosi ijayo.








0 COMMENTS:
Post a Comment