December 4, 2014


MTIBWA SUGAR.
Kikosi cha Mtibwa Sugar kinaendelea na maandalizi ya kucheza Ligi Kuu Bara kwa kuivaa Tesema, leo.



Mechi hiyo inapigwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kujiweka fiti.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amesema wanaendelea na maandalizi na baada ya mechi hiyo, kesho wataendelea na maandalizi jijini Dar.

"Leo tunacheza na Tesema, hii ni mechi ya kirafiki ili kuendelea kujiandaa na ligi. Kambi yetu kwa sasa iko hapa Dar es Salaam kwa muda," alisema Maxime.

Mtibwa Sugar na Simba ndiyo timu ambazo hazijapoteza mchezo katika mechi saba za Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic