Kiungo nyota wa Yanga, Simon Msuva amesema
amedhamiria kwa nguvu kufuata nyayo za mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana
Samatta.
Nyota huyo wa Yanga amesema anataka kuondoka
na kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania kama ilivyo kwa Samatta na
baadaye apate mafanikio kimaisha.
Katika mahojiano na SALEHJEMBE mwanzoni mwa wiki hii,
Msuva amesema anataka kupata mafanikio kama yale ya Samatta au mwenzake, Thomas
Ulimwengu ambao wanakipiga Mazembe.
Msuva amesema alipofikia Samatta ni sehemu
ya kuonyesha kwamba kuna mabadiliko kimaisha na ndicho kitu anachokitaka ikiwa
ni sehemu ya ndoto yake ya kufanikiwa kisoka na baadaye kimaisha.
SALEHJEMBE: Kipi hasa kinachokuvutia
kutokana na Samatta kihatua?
Msuva: Unaweza kusema maisha yamebadilika,
haishi tena kama ilivyokuwa mwanzo, kuna vitu anapata na awali hakuwa
akivipata, naweza kusema tayari yuko level nyingine.
SALEHJEMBE: Maana yake unataka kwenda
kucheza TP Mazembe?
Msuva: Yote hiyo ni mipango hapa duniani pia
ni mipango ya Mungu. Kikubwa ninataka kutoka nje ya Tanzania na kucheza.
SALEHJEMBE:Unalenga Ulaya au hata kokote
Afrika?
Msuva: Ikiwa Ulaya itakuwa vizuri, lakini
ikiwa Afrika pia ni sawa. Unaona Samatta, Ulimwengu wamefanikiwa wako Afrika.
Lakini kuna Mwinyi Kazimoto, yuko Qatar pia anaendelea vizuri, ninatamani sana
kufika huko. Ninaamini si siku nyingi.
SALEHJEMBE:Unaposema si siku nyingi, una
maanisha tayari kuna mipango imeanza kufanyika?
Msuva: Hilo linawezekana lipo, lakini si
vizuri kusema sasa. Ila kikubwa kwangu namshukuru Mungu nina afya njema.
SALEHJEMBE:Nje si lelemama!
Msuva: Hata Yanga si lelemama, ninafanya
mazoezi ya timu, ninafanya mazoezi ya ziada, wakati mwingine asubuhi au jioni
nikiwa na timu yangu ya wana wa mtaani.
SALEHJEMBE:Kuhusiana na wewe kuanza au kukaa
nje. Unajiona bora ukiingia au ukianza?
Msuva: (Kicheko), hakuna mchezaji anayependa
kukaa benchi lakini hilo ni suala la mwalimu. Mimi najiandaa kwa hali yoyote,
hata nikipewa dakika 20, najituma vilivyo. Sitaki niingie halafu nishindwe ili
watu waseme kwamba nastahili benchi.
Mungu akuongoze katika ndoto zako
ReplyDeleteUsikate tamaa, jibiidishe mazoezini, na ujitambue
ReplyDelete