December 30, 2014

MOJA YA NDEGE ZA KISASA ZA QATAR...
 Kocha mpya wa Simba, Goran Kuponovic anatarajia kutua nchini saa 1:30 akiwa ndani ya ndege ya Qatar Airways.

Ingawa imekuwa ni siri, lakini kocha huyo raia wa Serbia ambaye anatarajia kuchukua nafasi ya Patrick Phiri atapokelewa na viongozi wa Simba na baada ya kupumzika, atafanya nao mazungumza.


GORAN...
Baada ya mazungumzo na kusaini kujiunga nayo, kocha huyo wa zamani wa Polisi Rwanda na Dong Tam Long ya Vietnam, atajiunga na kikosi cha Simba kilicho Zanzibar kwa ajili ya michuano ya mapinduzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic