Hatimaye dirisha la usajili limefungwa huku ikionyesha Mwadui FC ya Shinyanga ikiwa imesajili wachezaji wengi zaidi.
Mwadui imesajili wachezaji wanne katika siku moja ya mwisho ambao ni Razak Khalfan kutoka Coastal Union, Uhuru Selemani, Joram Mgeveke (Simba) na Mohammed Mkweche.
KESSY |
Lakini wakongwe Simba na Yanga nao wamefunga dirisha kwa kulamba bingo.
Yanga imemnasa Amissi Tambwe aliyekuwa ameachwa Simba na kumsainisha mwaka mmoja, huku Simba ikimalizana na beki mbishi, Mohammed Kessy ambaye amesaini mwaka mmoja na nusu.
Stand United imefaidika na usajili wa Haruna Chanongo. Huenda kuna wengi waliosajiliwa, lakini tuliofanikiwa kwa leo ni hao.
Zaidi tutaendelea kesho.
HII MTANI JEMBE SASA NISHIIDAAAH YAANI KILA MWAKA INAKULA KICHWA CHA KOCHA WA YANGA!!!
ReplyDeleteNIONAVYO MIMINI KAMA MAXIMO ALIKUJA YANGA KUSHUSHA HESHIMA YAKE MAANA YANGA SI WAVUMILIVU KAMA ILIVYOKUWA TFF YA TENGA KUMVUMILIA MAXIMO WAKATI ANAJENGA TIMU. MAXIMO ALILIJUA HILO LAKINI SIJUI NI NINI KILIMFANYA ASILIPIME NA KUAMUA KUTOKUJA AU LABDA NGUVU YA PESA ZA YANGA? LAKINI KIUHALISIA NI KWAMBA SIFA YA MAXIMO KWA WATANZANIA NDO KWISHA NA ZILE SIFA ZOOOTE ALIZOPATA ZIMEVURUGWA NA MTANI JEMBE. KWELI UKIJA YANGA KUFANYA KAZI UJUE UTAPOKEWA KWA MBWEMBWE NA UTATIMULIWA KWA MBWEMBWE PIA.
BYEBYE MAXIMO YANGA HATUHITAJI WALIMU WA KUJENGA TIMU TUNA PESA TUNAHITAJI KUNUNUA WACHEZAJI NA KUMUUA MNYAMA BASI MAMBO YA KUJENGA TIMU HUKO HUKO TFF!