Kiungo mkabaji wa Simba,
Jonas Mkude amepewa mapumziko ya siku tatu kutokana na kusumbuliwa na Ugonjwa wa
Malaria uliomuanza juzi Alhamisi.
Mkude alikumbwa na ugonjwa
huo wakati akiwa kambini na wenzake kwenye kikosi hicho kilichopo kambini
katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ‘JKT’ maeneo ya Mbweni nje kidogo ya Jiji
la Dar.
Simba inatarajiwa kuvaana na
Yanga kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga itakayopigwa Desemba 13, mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema kuwa kwa sasa Mkude anaendelea vizuri na
wanatarajia atarudi kwenye hali yake baada ya siku tatu.
“Mkude anaendelea vizuri baada ya jana (juzi)
kupimwa na kukutwa ana wadudu wawili wa malaria na tunatarajia kwa muda wa siku
tatu tuliompa ili apumzike atakuwa fiti na kujiunga na wenzake kuendelea na
mazoezi,” alisema Gembe.







0 COMMENTS:
Post a Comment