Kiungo wa West Ham, Alex Song amestaafu
kuichezea timu yake ya taifa ya Cameroon.
Song amestaafu na kutundika kwenye mtandao
kwamba ameamua kutoichezea Cameroon kabisa.
Hali hiyo imeamsha furaha kwa Kocha wa West
Ham, Sam Allardyce ambaye anasikia faraja kubwa kuendelea kumtumia kwenye Ligi
Kuu England.
Hata hivyo, Allardyce amekuwa makini
ushiriki wake katika jambo hilo akihofia Fifa kuona amemshinikiza.
Song anaonekana kuwa na hasira ya kuachwa
kwenye Kombe la Mataifa Afrika lakini pia mfarakano na kocha wake ambaye
alimtaka kuomba radhi baada ya kupiga kiwiko kwenye Kombe la Dunia nchini
Brazil.
Lakini Song hakufanya hivyo, mwisho akaamua
kumtema hali iliyozua utata huo.









0 COMMENTS:
Post a Comment