Na Saad Mwinshehe, Zanzibar
Kocha mpya wa Simba, Goran Kopunivic amesema
Ligi kuu Bara ni muhimu zaidi kwao, lakini wanataka kushinda zaidi katika mechi
za Kombe la Mapinduzi.
Kopunovic amesema, amezungumza na wachezaji
wake na kuwaambia ni muhimu kushinda mechi ya leo dhidi ya Taifa ya Jang’ombe.
“Wanajua tunatakiwa kushinda, ni muhimu sana
kwa kuwa ni mechi ya mashindano yanayoheshimika. Lakini hii ni sehemu ya
maandalizi yetu ya ligi.
“Tukishinda mechi ya leo (dhidi ya Jang’ombe),
maana yake tunapata nafasi ya kusonga mbele na tunaweza kupata nafasi nyingine
ya kuendelea kujiandaa.
“Hivyo ni vizuri kushinda kila mechi ya
Mapinduzi ili kujiimarisha kwa ajili ya ligi,” alisema Kopunovic dakika chache
kabla ya mechi kati ya Simba dhidi ya Taifa Jang’ombe.
Mechi hiyo ya robo fainali ya Kombe la
Mapinduzi inaendelea kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.








0 COMMENTS:
Post a Comment