Azam FC inalazimika kulifanyia kazi suala la mikwaju ya penalti baada ya kutolewa kwa mara ya tatu katika michuano mbalimbali kwa changamoto hiyo.
Azam FC imetolewa na Mtibwa Sugar katika hatua ya robo fainali ya michuano Kombe la Mapinduzi.
Meneja wa Azam FC, Jemedari Said amesema wameona ni suala la kulifanyia kazi.
"Mara ya tatu sasa tunatolewa kwa mikwaju ya penalti. Nakumbu Simba walitutoa, halafu kwenye Kagame tukatolewa na El Merreikh na sasa Mtibwa Sugar.
"Ni sehemu ya kuangalia kuna tatizo na kipi cha kulifanyia kazi kwa ufasaha na hii ndiyo maana ya kushiriki michuano mbalimbali.
"Kuhusiana na michuano ya Mapinduzi tunaitumia kama sehemu yetu ya kujifunza na wala si kutafuta nani mchawi au ametufungisha," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment