Baada ya matukio mbalimbali ya waamuzi kupigwa katika viwanja
tofauti katika mechi za Ligi Daraja la Kwanza, Chama cha Waamuzi wa Soka
Tanzania (Frat), kimelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwawekea bima
waamuzi.
Akizungumza kwa uchungu kutoka mkoani Shinyanga,
Mwenyekiti wa Frat, Mwalimu Nassoro, alisema inasikitisha kuona waamuzi
wanapigwa kutokana na sababu ambazo hazieleweki huku akiwataka TFF kuwa na
sheria kali pamoja na kuwawekea bima waamuzi.
“Nimeshangaa sana matukio hayo, ajabu hata askari ambao wanatakiwa
kulinda amani nao ndiyo wanageuka kuwa wa kuwapiga waamuzi, wanataka waamuzi
tukimbilie wapi?” alihoji kiongozi huyo.
Aliongeza kuwa, Frat inalaani matukio hayo yakiwemo ya timu za Polisi
Dodoma na Polisi Mara kuwashambulia waamuzi.








0 COMMENTS:
Post a Comment