Kitendo cha kipa wa Simba, Peter Manyika
kutolewa katika dakika za mwisho kisha nafasi yake kuchukuliwa na Ivo Mapunda
wakati wa fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar, kimezungumzwa na
mzazi wa chipukizi huyo, Manyika Peter.
Baba mzazi wa kipa huyo, amesema kuwa mwanaye
ilikuwa lazima atolewe kwa kuwa kiwango chake kimeshuka katika siku za hivi
karibuni, ndiyo maana akatolewa dakika chache kabla ya mechi kuamuliwa kwa
matuta.
Katika mechi hiyo, Simba ilitwaa ubingwa kwa
penalti 4-3 huku Mapunda akiibuka shujaa baada ya kupangua mkwaju wa mwisho
uliopigwa na Vincent Barnabas.
“Ilikuwa afadhari Manyika kutodaka penalti kwa
sababu kiwango chake hakikuwa kizuri, kwa ninavyomfahamu naona ameshuka kiwango
tofauti na alipokwenda Simba mara ya kwanza.
“Nafikiri sasa ana nafasi ya kurejesha kiwango
chake kupitia mazoezi,” alisema Manyika.
Manyika ni kati ya makipa makinda nchini
ambao wanafanya vema na ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars Maboresho.








0 COMMENTS:
Post a Comment