Kiungo na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Warundi, Amissi Tambwe na Pierre Kwizera, wanatarajia
kuiburuza tumu hiyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu madai yao ya
kuvunja mkataba ambayo Simba haijawalipa.
Wachezaji
hao walisitishiwa mikataba yao na kuahidiwa kulipwa, lakini wanasema
hawajalipwa mpaka sasa, huku Tambwe akitua Yanga, Kwizera akirudi Burundi.
Tambwe
amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kuchoshwa
na uongo wa viongozi wa Simba dhidi yao kila wanapowasiliana nao.
“Hali
hiyo imetuchosha na tunaona Simba siyo wakweli, Jumatatu ijayo (keshokutwa)
tutapeleka malalamiko yetu TFF ili waweze kutusaidia kupata haki yetu.
“Wakati
tunajiunga na timu hiyo walitupokea kwa mikono miwili lakini sasa hatuwaelewi
kabisa jinsi wanavyotufanyia. Walipotuita kuwa wanataka kutuacha tulikubaliana
nao vizuri, hivyo wanapaswa kuzingatia makubaliano hayo na siyo kutuzungusha,”
alisema Tambwe.
Kila
wanapoulizwa juu ya suala hilo, viongozi wa Simba wamekuwa wakijibu kwa ufupi
kuwa wameshawalipa wachezaji hao.







0 COMMENTS:
Post a Comment