January 8, 2015


Pamoja na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Taifa ya Jang'ombe, jana, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema bado safu yake ya ushambuliaji haijakaa vizuri.


Kopunovic amesema amaefurahishwa na ushindi huo kwenye robo fainali ya Kombe la Mapinduzi, lakini bado anahitaji kufanya jambo.

"Utaona tumepoteza nafasi nyingi sana, nafikiri tunahitaji kuongeza umakini zaidi ili kufunga mabao mengi zaidi.

"Kitu kizuri wachezaji walisikiliza na kuelewa wakati wa mapumziko. Kipindi cha pili wakabadilisha mambo.

"Lakini tunapaswa kucheza kama ilivyokuwa kipindi cha pili. Mechi za mtoano zinakuwa tofauti, zina presha hivyo ni lazima kujua nini cha kufanya," alisema Kopunovic.

Simba ilionyesha soka safi na kuitungua Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0 ukiwa ni ushinda wa kwanza mkubwa wa timu hiyo baada ya kuanza michuano hiyo kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na baadaye ikashinda mechi mbili mfululizo lakini zote kwa bao moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic