Na Zaidi Mwinshehe, Zanzibar
Uongozi wa Yanga
rasmi umemtema kipa Juma Kaseja na kumtakia kila la kheri aendako.
Akizungumza mjini hapa, Mkurugenzi wa
Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema Kaseja amevunja mkataba kutokana na
kutokwenda mazoezini kwa saa 48.
“Kaseja haidai
Yanga na fedha zake aliishalipwa, tarehe zinaonyesha siku fedha hizo
zilipolipwa.
“Pia katika
mkataba hakukuwa na sehemu inaonyesha ni lazima Kaseja alipwe siku fulani
lakini ilikuwa ni lazima alipwe ndani ya kipindi cha mkataba.
“Yeye aliamua
kususa kuja kazini, jambo ambalo lilivunja mkataba wake na Yanga.
“Kwa kuwa hatudai,
tumeona ni vema kumuachia aende andako na tunamtakia kila la kheri kama klabu
ya Yanga,” alisema Muro.
Kaseja alijiunga
na Yanga baada ya kuwa huru kutokana na Simba kumuacha.
Lakini aliamua
kususia mazoezi baada ya Yanga kuchelewa kumlipa fedha zake za usajili
zilizosalia.
Baada ya Kaseja
kulipwa fedha alizokuwa akidai, aliandika barua kueleza amepokea fedha zake na
alikuwa tayari kurudi kazini, lakini uongozi wa Yanga haukumjibu.
Kutokana na kuona
hajibiwi, Kaseja alikwenda mazoezini lakini Kocha Marcio Maximo akamkataza kwa
kusisitiza lazima awasiliane na uongozi wa Yanga.
Kaseja ni kati ya
makipa wakongwe nchini ambao wamewahi kung’ara akiwa Simba na timu ya taifa,
Taifa Stars.








0 COMMENTS:
Post a Comment