Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema angependa kuona kikosi chake kinashusha asilimia ya upotezaji nafasi.
Pluijm amesema bado anakerwa sana na namna timu yake inavyopoteza nafasi licha ya kutengeneza kwa wingi.
"Hauwezi kushinda kama hautumii nafasi unazozipata. Kwa mfumo, lazima utengeneze nafasi halafu uzitumie na hiyo ndiyo maana ya ushindi.
"Tulipoteza nafasi nyingi katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting. Tulifanya hivyo pia katika michuano ya Mapinduzi.
"Tumerekebisha lakini bado inaonekana ni tatizo kubwa. Naendelea kulifanyia kazi," alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment