Kocha Goran Kopunovic
ameendelea kukinoa kikosi chake leo kwenye Uwanja wa Boko Union jijini Dar.
Kopunovic amesema
wanaendelea na mazoezi kujiimarisha zaidi ili kuwa tayari dhidi ya timu yoyote
mbele yao.
“Tutakuwa tayari dhidi ya
timu yoyote itakayokuwa mbele yetu.
“Tunajua ligi ni ngumu,
lakini kujiandaa ni jambo bora zaidi kwa kuwa unakuwa tayari kwa lolote,”
alisema.
Tayari Simba imeishashinda
mechi moja ikiwa ni ya kwanza kwa kocha huyo ya Ligi Kuu Bara pale ilipoitwanga
Ndanda FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment