Kocha Mkuu wa Yanga, Hans
van der Pluijm amesema wamejifunza mengi katika michuano ya Mapinduzi na
yatawasaidia.
Pluijm raia wa Uholanzi
amesema kumekuwa na mengi na yatawasaidia kwenye Ligi Kuu Bara na michuano ya
Kombe la Shirikisho.
“Tumecheza michuano hiyo
kwa mafanikio makubwa, kutolewa linaweza lisiwe jambo namba moja.
“Tumejifunza na kugundua
matatizo kadhaa ya msingi ambayo tunayafanyia kazi. Kikubwa ni nini cha kufanya
baada ya hapo.
“Tuna michuano ya ligi na
ile ya kimataifa, hivyo lazima tujue tuna mzigo mkubwa mbele yetu,” alisema
Pluijm.
Yanga ilitolewa katika
hatua ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi huku ikiwa ndiyo timu inaongoza kwa
kufunga mabao mengi na kuibuka na ushindi wa mabao manne mara mbili mfululizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment