Baada ya kutojulikana kuwa nani atacheza na Simba katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi, sasa kila kitu hadharani.
Simba itaivaa Taifa ya Jang'ombe katika mechi ya michuano hiyo hatua ya robo fainali.
Mechi hiyo itachezwa saa 2 usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Siku inayofuata yaani keshokubwa, mechi nyingine ya robo fainali itapigwa jioni, nayo ni Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mechi hiyo inaaminika kuwa moja ya zile ngumu na safi za michuano ya Mapinduzi.







0 COMMENTS:
Post a Comment