January 6, 2015


Yanga imemaliza hatua ya makundi kwa kuwa na pointi 9 baada ya kupata ushindi wa tatu mfululizo.

Yanga imeifunga Shaba kwa bao 1-0 katika mechi ngumu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Pamoja na kushambulia sana na kukosa sana, Yanga walilazimika kusubiri hadi dakika ya 86 wakati Andrey Coutinho alipofunga bao kwa kichwa akiunganisha krosi ya Simon Msuva.


Yanga walipoteza nafasi zaidi ya tano za wazi za kufunga kupitia kwa Mrisho Ngassa, Simon Msuva na Amissi Tambwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic