January 6, 2015



Unamkumbuka yule straika aliyebatizwa jina la “bonge”, alikwenda kufanya mazoezi Yanga, Kocha Marcio Maximo akamtosa, sasa yuko Hispania.



Suleiman Abdallah Mbarouk amesema anaendelea vizuri katika klabu yake ya daraja la pili ua Jerez ambayo imempeleka kwa mkopo Fosehill.

“Huku naendelea vizuri kabisa, sasa nimerudi Uingereza kwa muda kwa ajili ya mapumziko ya mwanzo wa msimu.

“Kitu ambacho ninaweza kusema ni masikitiko yangu kuhusiana na yule aliyekuwa kocha wa Yanga, (Marcio) Maximo. Alinifanyia kitu kibaya kwa kushindwa kunipa nafasi hata kidogo kuonyesha uwezo wangu.

“Nilikuja Yanga kufanya majaribio, lakini hakunipa nafasi hata kidogo. Badala yake alionyesha hofu kama ningefanikiwa basi ningeweza kuwanyima nafasi ndugu zake Wabrazil.

“Wanasema mimi bonge, vipi nacheza Hispania, nacheza England? Kwani soka la England na kwetu Afrika lipi lipo juu,” alisema.

“Nasikia kafukuzwa, ila alinionea sana. Sasa nacheza kwenye timu yangu, nimecheza mechi tisa, nimefunga mabao saba. Nitarudi Spain Januari 9 ili kuendelea na kazi.”

Mbarouk alifanya majaribio Yanga kwa siku moja tu kabla ya Maximo kumzuia kuendelea kwa madai alikuwa na umbo kubwa.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic