Straika nyota wa Yanga, Amissi Tambwe ameamua kujipanga upya ili kuhakikisha anakuwa fiti kwa mbinu mpya za kufunga mabao.
Tambwe alikuwa kati ya washambuliaji waliopoteza nafasi nyingi za kufunga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Tayari Tambwe ameichezea Yanga mechi moja ya Ligi Kuu Bara na kuifungia bao moja.
Straika huyo
amesema anatamani malengo yake msimu huu pia yaweze kutimia kama ilivyokuwa
msimu uliopita.
“Mipango yangu kwa sasa ni kuhakikisha nakuwa
na mbinu mpya ambayo itanisaidia katika kuifungia timu yangu mabao mengi na
kuiwezesha kuwa juu, siwezi kukata tamaa mapema zaidi ni kuomba Mungu niwe
mzima siku zote kuweza kutimiza malengo yangu.
“Japo si lazima nifunge peke yangu lakini
nitashirikiana na wenzangu katika kikosi chetu hata kwa kutoa pasi, akifunga
mwingine si tatizo kwa sababu lengo letu ni moja, kuifanya timu yetu ipate
pointi katika kila mchezo,” alisema Tambwe.







0 COMMENTS:
Post a Comment