February 20, 2015


Mario Balotelli haishi vituko, ameisaidia Liverpool kuibuka na ushindi bao 1-0 dhidi ya Besiktas ua Uturuki katika mechi ya Ligi ya Europa.


Balotelli amefunga lakini bado ni shidaa, maana alimpokonya mshambuliaji mwenzake Danny Sturridge mpira.
 
Wakati ilionekana mwamuzi Henderson alitaka kumpa Sturridge lakii Balotelli akaonekana kutowaamini wenzake.

Ilikuwa ni dakika ya 85, alitaka uhakika. Hakujali kama Sturridge au wengine watachukia, akachukua na kupiga na kweli akafunga.


Wakati Balotelli anashangilia na wengine, wengine walikuwa wanafanya kazi ya kumpoza Sturridge ambaye alikuwa na jazba.

Nahodha hasa wa Liverpool, Steven Gerrard alikuwa akifanya uchambuzi kwenye runinga na ITV. Kuhusu hilo, alimpongeza Balotelli kwa kufunga lakini akasisitiza, haikuwa sahihi kugombea mpira kwa kuwa ilionyesha ni utovu wa nidhamu.

Liverpool: Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Ibe, Henderson, Allen (Lovren 63), Moreno, Lallana (Sterling 77), Sturridge, Coutinho (Balotelli 63)
Subs not used: Ward, Lambert, Manquillo, Borini
Booked: Lovren 
Goals: Balotelli 85' (pen) 

Besiktas: Gonen, Kurtulus, Franco, Gulum, Ramon, Hutchinson, Kavlak, Tore, Sosa (Ozyakup 60), Sahan (Frei 72), Ba
Subs not used: Fidayeo, Pektemek, Arslan, Uysal, Opare
Booked: Gulum, Kurtulus, Motta, Franco
Referee: Szymon Marciniak (Poland) 













0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic