| UONGOZI WA JUU WA SIMBA; MWENYEKITI EVANS AVEVA (KUSHOTO) NA MAKAMU WAKE, GEOFREY NYANGE 'KABURU' |
Uongozi wa Simba pamoja umefikia uamuzi wa kumzuia mmoja wa viongozi
wake kufika kambini kwa maslahi ya timu.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kiongozi huyo
mwanandamizi, amezuiwa na tayari amepewa taarifa.
“Kweli kuna hatua zimechukuliwa na uongozi, tumeona kila anapokwenda
linakuwa ni tatizo kubwa.
“Amekuwa akichangia kuwavuruga wachezaji, hivyo tulichoamua asiende
kambini timu itakapokuwa Dar es Salaam au nje ya mkoa,” kilieleza chanzo na
kuendelea:
“Mara kadhaa tumepata malalamiko, hata wachezaji wamekuwa wakilaumu
sana kwamba anawachanganya na wakati mwingine anawaambia maneno ya kashfa, kitu
kinachowavunja nguvu.
“Wachezaji pia wamelalamika amekuwa akiwapiga vita kwa kumwambia
kocha kuwa wao hawafai lakini wanapokutana naye anawachekea.”
Hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic alifunguka kuwa
kuna kiongozi amekuwa akimpangia timu na kumuonyesha fomesheni ya kutumia.
Baadaye Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans
Poppe akasema kocha alisema alikataa ushauri wa kiongozi huyo, hivyo haikuwa
kulazimisha badala yake ni ushauri.







0 COMMENTS:
Post a Comment