February 11, 2015


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho, ametamka kuwa hana raha na amani baada ya hadi sasa kuifungia Yanga bao moja tu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.


Kauli hiyo, ameitoa mara baada ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mrisho Ngassa, kupachika mabao mawili wakati walipocheza na Mtibwa Sugar katika mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0.

Coutinho amesema kuwa hajisikii vizuri kuona akiendelea kuichezea timu hiyo bila ya kufunga mabao, hivyo amejipanga kwa kuhakikisha anaitumia vyema kila nafasi atakayoipata ndani ya uwanja kufunga mabao.

Coutihno alisema, anakosa usingizi kila anapofikiria ameshindwa kufunga mabao, hali inayomfanya ajione hana mchango katika timu hiyo inayoongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 25.

“Ninashindwa kuelewa sababu ya kushindwa kufunga mabao, haiwezekani hadi kufikia raundi hii nifunge bao moja pekee huku wenzangu wakiendelea kufunga mabao.

“Ninajiona ni mchezaji nisiyekuwa na mchango kwenye timu, hivyo nimepanga katika mechi zijazo za ligi kuu, nihakikishe ninafunga mabao kwa kila nafasi nitakayoipata.


“Nitaongeza umakini mkubwa kiukweli katika mechi hizo za ligi kuu, ninaomba ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzangu kwenye timu, kwa sasa sijisikii vizuri,” alisema Coutinho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic