Huku mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania
Bara ukiwa unaendelea, mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, ndiye
aliyewafunika Waganda wenzake mpaka sasa kwa kuwa na mabao manne.
Ligi Kuu Tanzania Bara ina wachezaji wengi
kutoka Uganda na mshambuliaji huyo ndiye aliyeonekana kuwa kinara wa kupachika
mabao.
Katika listi hiyo, kuna wachezaji Dan
Sserunkuma (Simba), Lutimba Yayo (Coastal Union) na Simon Sserunkuma (Simba).
Hata hivyo, kwa msimu uliopita mpaka ligi
inamalizika, Hamisi Kiiza ndiye alikuwa Mganda pekee mwenye mabao mengi ambapo
alitikisa nyavu mara 12.
Okwi ambaye ameanza kuitumikia Simba tangu
mwanzoni mwa msimu huu, mpaka sasa ligi ikiwa raundi ya 14, amefanikiwa kufunga
mabao manne.
Mshambuliaji huyo kwa sasa anafukuzana na
Mganda mwenzake Danny wa kikosi hicho ambaye ana mabao matatu na amecheza mechi
sita mpaka sasa.
Kwa upande wa Yayo, yeye ameifungia timu yake
bao moja na msimu uliopita alimaliza ligi akiwa na bao moja. Mganda wa Simba,
Simon, kwenye michezo sita hajafunga bao hata moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment