Straika wa Yanga raia wa Liberia,
Kpah Sherman, mpaka sasa amecheza
dakika 540, ambazo ni sawa na mechi sita za Ligi Kuu Tanzania Bara bila
kufunga bao lolote katika kikosi chake hicho.
Sherman alisajiliwa katika kipindi cha dirisha
dogo akichukua nafasi ya aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Mganda, Hamis
Kiiza, ambaye msimu uliopita alimaliza ligi akiwa na mabao 12.
Katika kikosi cha Yanga ambacho kina
washambuliaji wa kigeni wawili pekee, bado wageni ambao ni Sherman pamoja na
Mrundi, Amissi Tambwe wanaonekana kusuasua kutokana na kushindwa kutikisa nyavu
mara nyingi.
Tambwe mpaka sasa ana mabao mawili, moja
alifunga akiwa Simba na moja kwa timu yake ya sasa na wote walisajiliwa kipindi
cha usajili wa dirisha dogo msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment