February 10, 2015


KOCHA TEGETE AKIWA NA KIKOSI CHA TOTO...
Ni kazi kwelikweli katika Kundi B la Ligi Daraja la Kwanza, sasa timu tatu zinafukuzana kuwania nafasi mbili za kupanda Ligi Kuu Bara.



Ushindi wa leo dhidi ya Polisi Tabora wa Mwadui FC inayonolewa na Jamhuri Kihwelo, umewafanya wawe katika nafasi nzuri ya kupanda lakini lazima washinde katika mechi yao ya mwisho kwa kuwa tayari wana pointi 43.

Wakati wao wana pointi hizo, JKT Oljoro, imeshinda mechi yake dhidi ya Rhino umewafanya wafikishe pointi 41.

Lakini Toto inayonolewa na John Tegete, tayari ina pointi 39, lakini mechi yake dhidi ya Geita imevunjika na kila dalili inaonyesha watapewa pointi tatu na kufikisha 42.

Maana yake majibu ya nani anapanda kati ya timu hizo tatu yatapatikana katika mechi ya mwisho.

Mwadui FC na Toto zinaweza kuwa na uhakika zaidi iwapo zitashinda na iwapo mmoja wao atateleza na kumpa nafasi Oljoro ashinde, basi itakuwa mdudu kaingiaje ndani ya kokwa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic