Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa
kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42
amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.
Kati ya hao ni Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Wilfred Mwakalebela ambaye ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mwakalebela ameula baada ya Rais Kikwete kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI
leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema
mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana
na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya
watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa
uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha
vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani
wakuu wa wilaya 42.
Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima
anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema
(Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda
Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.
Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi
(Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto),
Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita
(Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea
Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na
Stephen Zelothe (Musoma).
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro);
Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta
(Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma
Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).
Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini
watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro;
Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa);
Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo);
Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao
umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji
Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido);
Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus
Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu
(Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi);
Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati)
na Elias Goroi (Rorya).







0 COMMENTS:
Post a Comment