Simba
imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Moro katika mechi
ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Simba
ilifanikiwa kufunga bao katika kila kipindi huku ikionyesha soka safi.
Bao la kwanza
katika kipindi cha kwanza lilifungwa na Ajibu ambaye awali alipoteza nafasi
nzuri ya kufunga.
Polisi hawakuwa
walahisi kwa kuwa walionyesha soka safi lakini nao hawakuwa makini katika
umaliziaji.
Kipindi cha
pili, Elius Maguri aliyeisumbua sana safu ya ulinzi ya Polisi aliifungia Simba
bao la pili na kuwavunja nguvu Polisi.
Simba
walionekana kuwa si wale kwani waliendelea kushambulia hata mwisho wa kipindi
cha pili.
Hata hivyo,
Polisi walikuwa wakijibu mara kadhaa lakini safu ya ulinzi ya Juuko Murishid
ilipambana kuondoa hatari zote.







0 COMMENTS:
Post a Comment